Wanaokwamisha uwekezaji EPZA kuondoshwa

0
243

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Karibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara Dotto James kuwahamisha mara moja Watumishi wote wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) waliosababisha hasara katika eneo hilo.

Akiwa katika ziara ya kutembelea eneo la EPZA Mabibo mkoani Dar es salaam, Waziri Mkuu Majaliwa amekagua uzalishaji katika eneo hilo na kuagiza kuhamishwa kituo cha kazi Watumishi wote walioshiriki kukwamisha uwekezaji kwenye eneo hilo.

Ameongeza kuwa maeneo ya kuwekeza ndani ya EPZA yapo, lakini baadhi ya Watumishi wamekuwa wakiwakwamisha Wawekezaji.

Akitolea mfano wa ucheleweshwaji wa Wawekezaji katika eneo hilo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Mwanasheria wa EPZA amekuwa kikwazo kwa Wawekezaji, hali inayokwamisha uwekezaji hapa nchini

“Mwanasheria hapa ni Sara, huyu amekuwa akikwamisha sana uwekezaji anachelewesha maombi ya Wawekezaji kwa kisingizio cha sheria, Katibu Mkuu huyu muhamishe ahame hapa.” ameagiza Waziri Mkuu Majaliwa.

Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo alimueleza Waziri Mkuu Majaliwa kuwa eneo la EPZA limekuwa na changamoto kubwa za kiutendaji, hali inayokwamisha uwekezaji katika eneo hilo