Wanaokata mabomba Msomera waonywa

0
189

Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Albert Msando amesema atachukua hatua za kisheria kwa mtu au kikundi kitakachobainika kujihusisha na ukataji wa mabomba ya maji kwenye kijiji cha Msomera wilayani humo.

Msando ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya ugawaji wa majiko banifu na mitungi ya gesi ya kupikia 1,500 iliyotolewa na Serikali chini ya Wizara ya Nishati pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amesema wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Serikali ambao wanaharibu miundombinu ya maji iliyojengwa na Serikali katika eneo hilo ambalo tayari Serikali imejenga mabomba 66 ya maji kwa ajili ya maji safi, bwawa kubwa la maji pamoja na mbauti tano kwa ajili ya kunyweshea mifugo.

Kijiji cha Msomera kinakaliwa na wananchi waliohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro.