Wananchi wote mbioni kunufaika na bima ya afya

0
345

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema kuwa mpango wa serikali wa kuanzisha bima ya afya kwa wananchi wote upo katika hatua za mwisho.

Ummy Mwalimu ameyasema hayo wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Kiteto Koshuma (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka bungeni muswada wa sheria ya kuwataka wananchi wote kujiunga na mifuko ya taifa ya bima ya afya.

“Pindi serikali itakaporidhia mapendekezo hayo, suala hili litawasilishwa bungeni kujadiliwa na kufanyiwa maamuzi,” amesema Ummy.

Sheria hiyo itakapopitishwa itamlazimu kila mwananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya.

Wizara ya afya imesema kuwa inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria hiyo katika bunge la 12.