Wasomi wazikubali siku 100 za Rais

0
224

Katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa, vijana nchini wametakiwa kuwa wazalendo wa kweli wanapopewa dhamana ya uongozi katika nafasi mbalimbali walizoaminiwa na Rais.

Hayo yamesemwa na Profesa Eginald Mihayo wakati wa Kongamano la Siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan madarakani lililoandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine jijini Mwanza

Akichokoza mada ya mdahalo huo Profesa Mihanjo amesema kuna haja ya kuwepo masomo ya uzalendo mashuleni ili kujenga Taifa la wazalendo kwa nchi yao.

“Ili Taifa lilinde maslahi yake, lazima wawepo wazalendo wa kulinda maslahi hayo, sasa changamoto iliyopo ni kama vijana hawatapata uelewa wa uzalendo wa Taifa lao,” amesisitiza Mihanjo

Aidha, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Balozi Costa Mahalu amesema katika siku 100, Rais Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri katika sekta ya uwekezaji kwa kuwakaribisha wawekezaji ambao watasaidia ukuaji wa sekta ya uwekezaji na uchumi hapa nchini.

Fides Zakayo ni mwanafunzi wa wa chuo hicho ambaye amesema ndani ya siku 100 za Rais zimekuwa na manufaa makubwa kwa vijana hasa upande wa ajira mpya.