Wananchi watakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya Tehama

Mbio za Mwenge

0
178

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Luteni Josephine Mwambashi amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano katika kujiletea maendeleo.

Luteni Mwambashi ametoa rai hiyo mara baada kukagua kituo cha mpango wa matumizi sahihi ya Tehama kilichopo Wailes wilayani Temeke mkoani Dar es salaam wakati wa mbio za Mwenge kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo wilyani humo.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa Dunia kwa sasa imekuwa kama kijiji kutokana na matumizi makubwa ya tehema hivyo ni vyema wananchi watambue fursa zilizopo kwenye sekta hiyo katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Katika hatua nyingine Mwambashi amekataa kuweka jiwe la Msingi wa ujenzi wa barabara ya Nzasa Kilungule kuelekea Buza yenye urefu wa kilometa 7 unaoelezwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 19

Luteni Mwambashi amesema Mwenge wa Uhuru hauwezi kuweka jiwe la Msingi la mradi wa barabara hiyo na stendi ya mabasi Buza kutokana na kutokuwepo kwa taarifa sahihi zinazohusu malipo ya fidia walizolupwa wananchi na ujenzi wa mradi kwa ujumla ambao unaelezwa kugharimu Shilingi Bilioni 19.

Aidha kiongozi huyo ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke kutoa taarifa juu ya Mradi huo ili wote waliohusika na kuhujumu mradi huo sheria iweze kuchukua mkondo wake.

“Tumepitia taarifa za mradi huu na kugundua baadhi ya changamoto ikiwemo ya kukinzana kwa taarifa za fedha zilizotumika kwenye mradi huu, hivyo kutokana na changamoto hiyo Mwenge wa Uhuru hautazindua mradi huu na naagiza TAKUKURU kuchukua hatua kabla Mwenge haijakabidhiwa sehemu nyingine na waliohujumu fedha za mradi sheria itafuata mkondo wake,”Amesema kiongozi huyo.

Miradi 14 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32 imefanikiwa kutembelewa na kukaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 Wilyani Temeke.