Wananchi wachanga fedha kuwanusuru viongozi wa CHADEMA

0
199

Zaidi ya shilingi milioni 230 zimechangwa kwa ajili ya kuwatoa gerezani viongozi Saba wa Kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wakizungumza na  waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA Said Issa Mohammedi amesema kuwa, fedha hizo zimetokana na michango ya wananchi mbalimbali.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Kigaila Benson amesema  kuwa, baada ya kupatikana kwa fedha hizo uongozi wa chama hicho umependekeza kwanza kuwatoa viongozi watatu wa kike  ambao ni Ester Matiko, Halima Mdee na Ester Bulaya

Zaidi ya shilingi milioni mia moja zinahitajika ili kukamilisha pesa zinazotakiwa ili kufanikisha kutolewa kwa viongozi hao.