Wananchi waaswa kulinda miundombini ya Bomba la Gesi

0
163

Wananchi wanaoishi maeneo unapopita Mradi wa bomba la Gesi asilia kutoka Mkoani Mtwara mpaka Mkoa Dar es salaam wametakiwa kulinda miundombinu ya Bomba hilo.

Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati wa kufunga semina na waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kutoka shirika la Maendeleo ya Petroli nchini TPDC Maria Msellem amesema kuwa Jamii inapaswa kuhakikisha kuwa miundombinu ya mradi huo inakua salama kwakua inamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi

“Lengo letu ni kuwaomba na kuendelea kuwasihi jamii inayoishi katika maeneo ambayo miundombinu hii inapita kuwa walinzi na mabalozi wazuri kuhakiksha kwamba miundo mbinu inakua salama ili kuendeleza uzalishaji wa nishaji hiyo” ameongeza Mselemu

Aidha Mselem ameongeza kuwa Shirika hilo limeendelea kuwa na Mchango mkubwa katika uzalishaji wa umeme nchini huku akiitaka jamii kuwa tayari kwaajili ya fursa zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Mkoani Tanga nchini.

Pia, TPDC imesema kuwa kupitia kampuni tanzu ya TANOIL imefanikiwa kuhifadhi mafuta ambayo yanatosheleza kutoa huduma kwa wananchi kulingana na uhitaji wa nishati hiyo hapa nchini.

Nao baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki seminina hiyo wamewapongeza TPDC kwa kuandaa semina hiyo na kuahidi kutoa elimu na kuwahabarisha watanzania kwa kina juu ya nishati ya mafuta na Gesi asilia inayosimamiwa na Shirika hilo.