Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji anatarajiwa kuzindua zoezi la utoaji fidia kwa Wananchi 1, 142 wa vijiji vinne vya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe; watakaopisha miradi pacha ya makaa ya mawe na chuma.
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema,
tukio hilo litafanyika Juni 07, 2023.
Wananchi hao wanatarajiwa kulipwa zaidi ya shilingi Bilioni 15 na Milioni 400 zikiwa ni fidia na riba.
Mtaka amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kuwalipa fidia Wananchi hao, ambao walikuwa wakiisubiri kwa muda wa zaidi ya miaka 40.