Jamii imetakiwa kuwakumbuka watoto wenye uhitaji maalum ikiwemo watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali na kuwasaidia kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku
Wito huo umetolewa na waendesha baiskeli wakiongozwa na Zawadi Mwambi Miss Utalii Njombe 2020, kupitia Ushirikiano wa Zawadi Charity Sambaza Upendo unaowajumuisha wadau na waendesha baiskeli mbalimbali kutoka nchini Tanzania
Wanamichezo hao walianza kwa matembezi ya baiskeli kuanzia daraja la Tanzanite hadi katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Umra kilichopo magomeni mkoani Dar es salaam
Aidha viongozi wa kituo hicho cha Umra wamewashukuru waendesha baiskeli hao kwa zawadi hizo na kuwaomba wadau wa michezo na wanamichezo wengine kuiga mfano huo kwani huko wanaweza kupatikana vijana wenye vipaji katika sekta ya michezo nchini