Wanafunzi wote kulipwa Boom mwezi huu

0
162

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema wizara yake imepokea maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi kuhusu suala la fedha za kujikimu(Boom) kwa wanafunzi wa vyuo nchini na inalifanyia kazi suala hilo.

Akiwa katika ziara yake eneo la Usa River Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Dkt. Nchimbi aliiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha wanafunzi wa vyuo wanalipwa fedha hizo ifikapo mwishoni wa mwezi huu.

Profesa Mkenda ambaye ni Mbunge wa Rombo mkoani Kilimanjaro, akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa CCM mkoani humo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM amesema, wizara yake imepokea agizo hilo na watalitekeleza kabla ya mwisho wa mwezi huu.

“Ndugu Katibu Mkuu jana pale Arusha ulitoa maelekezo kuhusu suala la Boom na naomba nitumie nafasi hii kusema kuwa suala hilo tutalifanyia kazi na kabla ya muda ulioutoa wanafunzi wote nchini watakuwa wamelipwa”, ameahidi Profesa Mkenda