Wanafunzi waomba wabunge wawasaidie wafanye mitihani

0
229

Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali wanawatafuta wabunge kwa ajili ya kuwasaidia ili waweze kufanya mitihani.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na kusema wanawatafuta kwa lengo la kuwasaidia ada ili waruhusiwe kufanya mitihani.

Pia Spika wa Bunge ameishauri Wizara husika kuangalia namna bora ya wanafunzi kuweza kufanya mitihani na kama hawajamaliza ada waruhisiwe kisha kuzuiwa kupata matokeo hadi wakilip ada.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge ameshauri kuangalia namna bora ya sare za wanafunzi kwa maeneo husika kwani sehemu nyingine sare zinakuwa si rafiki mazingira husika.