Wanafunzi kidato cha Nne kuanza mitihani leo

0
115

Wanafunzi wa kidato cha nne nchini leo wanaanza mitihani yao pamoja na ile ya maarifa, mtihani unaofanyika katika jumla ya shule 5,212 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 1,794.

Jumla ya watahiniwa 566,840 wamesajiwa kufanya mtihani huo ambapo 535,001 ni wa shule na 31,839 ni watahiniwa wa kujitegemea.