Wanafunzi 436 Mtwara hawajaripoti shule

0
166

Wanafunzi Mia Nne na Thelathini na Sita (436) wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wilaya ya Mtwara  waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu  bado hawajaripoti shuleni.

Akizungumza na wadau wa elimu katika Halmashauri ya mji huo, Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Marco Gaguti, ameagiza juhudi za makusudi zifanyike  ikiwa ni pamoja na kuwasaka wazazi na walezi wenye watoto hao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Gaguti amesema haiwezekani mkoa huo uwe unaongoza  kwa uzalishaji wa zao la korosho halafu kwenye elimu unakuwa mkoa wa mwisho jambo ambalo amesema halikubaliki.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Mtwara Kiduma Mageni, amesema Halmashauri hiyo inachangamoto kubwa ya mdondoko wa wanafunzi nakwamba mkoa umeandaa  mikakati ili kuondoa hali.

Mageni ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuwaandalia vitabu vya mahudhirio maafisa elimu wa kata ili wawe wanatembelea katika shule zao kuangalia mahudhurio ya wanafunzi na kutoa mrejesho kupitia vitabu hivyo.

Wanafunzi hao hawajaripoti shule ikiwa inakaribia miezi miwili sasa toka kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari.