Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Mabalozi kufanyia kazi na kutoa taarifa ya mikataba na makubaliano yaliyofikiwa baina ya Tanzania na nchi zingine.
Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akiwaapisha Mabalozi Ikulu Chamwino, Dodoma na kuongeza kuwa mikabata na makubaliano hayo baada ya kusainiwa hufungiwa kwenye makabati na hakuna taarifa inayotolewa kuhusu utekelezaje wake wala ufuatiliaji.
Amewakumbusha Mabalozi aliowateua na kuwaapisha kufanya ufuatiliaji wa mipango inayoihusu nchi ya Tanzania kusudi pale wanapokwenda kuwasilisha hati za utambulisho kwa Viongozi wakuu wa nchi hizo waweze kukumbushiwa mipango hiyo.