Wanafamilia wafariki baada ya gari kusombwa na maji

0
216

Watu wanne wa familia moja wanasadikiwa kufariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kusombwa na maji katika barabara ya Arusha – Moshi.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela ameiambia TBC kwa njia ya siku kuwa gari aina ya Noah iliyokuwa imebeba wanafamilia sita imesombwa na maji katika eneo la King’ori mkoani humo na kusababisha vifo hivyo.

Huko mkoani Kilimanjaro katika mpaka wa mkoa huo na Arusha, mvua imeleta madhara ikiwa ni pamoja na huduma za usafiri kusimama kwa saa kadhaa.