Wanachama wa CCM waanza kuchukua fomu kuwania Urais

0
503

Zoezi la kuchukua fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ule wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao limeanza hii leo.

Taarifa ya CCM imesema kuwa zoezi hilo litakamilika Juni 30 mwaka huu ambapo kwa upande wa Bara fomu zinatolewa katika ofisi za CCM makao makuu jijini Dodoma na kwa upande wa Zanzibar fomu hizo zinatolewa katika ofisi kuu za CCM Kisiwandui.

Habari kutoka Zanzibar zinaeleza kuwa tayari Mbwana Juma Bakari amefungua dimba la kuchukua fomu za kuwania Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM katika ofisi kuu za CCM Kisiwandui.