Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, amejiondoa kwenye nafasi ya kuwania ujumbe wa Baraza la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA Council) kuwakilisha nchi za Afrika zinazozungumza Kiingereza.
Karia amefanya maamuzi hayo baada ya kushauriana na viongozi wenzake wa Baraza la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambapo yeye ni Rais aliamua kujiondoa ili awekeze nguvu TFF na baraza hilo.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Mawasiliano TFF imesema kutokana na kumuunga mkono Patrice Motsepe wa Afrika Kusini, ambaye ni mgombea pekee wa urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).