Walimu tuzingatie mitaala

0
186

Mwezeshaji wa mradi wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) Chacha Nsaho amesisitiza umuhimu wa walimu kuzingatia mitaala ya elimu iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwani inatoa mwongozo katika ufundishaji.

Amesema mitaala hiyo inawezesha kwenda na mifumo ya Kitaifa na Kimataifa, kwani inaeleza kuhusu mipango na maendeleo ya nchi, maendeleo ya sayansi na teknolojia na hivyo kuchangia kukua zaidi kwa sekta ya elimu nchini.

Mwezeshaji huyo wa mradi wa SEQUIP amewataka walimu wanapofundisha wawatengenezee wanafunzi uwezo wa kufikiri, kujitegemea na kujiamini huku wakihamasisha matumizi sahihi ya Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) shuleni, kutokana na duniani kubadilika na kutegemea uchumi wa kidigitali.

Alikuwa akizungumza katika mafunzo ya walimu kuhusu TEHAMA yanayotolewa chini ya mradi wa SEQUIP, ambayo yanaendelea katika Chuo cha Ualimu Butimba mkoani Mwanza.