Walimu matatani kwa tuhuma za kumtoa mimba Mwanafuzi

0
231

Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia Walimu wawili wa shule ya sekondari ya Mang’oto iliyopo wilayani Makete, kwa tuhuma za kumtoa mimba Mwanafunzi wa shule hiyo mwenye umri wa miaka 17.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe, – Hamis Issah amesema kuwa kati ya walimu hao, mmoja anayefahamika kwa jina la Ezekiel Thomas ndiye aliyempa ujauzito Mwanafunzi huo.

Mara baada ya kubaini Mwanafunzi huo ana ujauzito, Mwalimu Ezekiel Thomas alishirikiana na mwalimu mwenzake kumpeleka hospitali mwanafunzi huyo na kumtoa mimba hiyo.