Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa miikoa wapya tisa , kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa mikoa saba na wengine 10 wanabaki kwenye vituo vyao vya kazi.
Wakuu wa mikoa waliobakishwa katika vituo vyao vya kazi ni pamoja na Amos Makalla ambaye anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
John Mongella anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha na Mwanamvua Hoza Mrindoko anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi.
Wengine ni Charles Makongoro ambaye anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara na Zainab Telack anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Lindi.
Juma Homera anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na Thobias Andengenye anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma.
Sophia Mjema anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na
Balozi Batilda Burian anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora na Abubakar Kunenge anaendelea kuwa mkuu wa mkoa wa Pwani.