Katika mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, mbali na kuwateua wakuu wa mikoa wapya tisa, amewahamisha vituo vya kazi wakuu wa mikoa saba.
Waliohamishwa ni pamoja na
Anthony lMtaka ambaye amehamishwa na kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe akitokeaa mkoa wa Dodoma.
Queen Sendiga amehamishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa akitokea mkoani Iringa.
Waziri Waziri Kindamba amehamishiwa Songwe akitokea Njombe na Martin Shigella amehamishiwa mkoani Geita akitokea Morogoro.
Wengine waliohamishwa vituo vya kazi ni Omary Mgumba ambaye amehamishwa na kuwa mkuu wa mkoa wa Tanga akitokea Songwe.
Adam Malima amehamishiwa mkoani Mwanza akitokea Tanga na Rosemary Senyamule amehamishiwa Dodoma akitokea mkoa wa Geita.