Wilaya ya Kasulu ipo katika hatua za kuanza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutangaza mazao yanaotunzwa katika maghala maalumu yasioruhusu wadudu waharibifu kuingia na kuharibu mazao hayo, ili kumaliza tatizo la ulanguzi unaofanywa na madalali
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya ushauri ya Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Asulu Anange amesema mradi huo ni sehemu ya miradi inayogharamiwa na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia mpango wa pamoja wa kisaidia Kigoma.
Kupitia mradi huo wakulima watanufaika kwa kupata bei nzuri ya mazao yao na kuachana na walanguzi wanaojitokeza kipindi cha mavuno.