Wananchi wa Kenya leo wameanza rasmi kuaga mwili wa Rais mstaafu wa nchi hiyo Mwai Kibaki aliyefariki duniani wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 90.
Shughuli ya kuaga mwili wa Kibaki inafanyika katika ukumbi wa bunge jijini Nairobi, na itaendelea hadi siku ya Ijumaa ambapo Viongozi na wageni kutoka taasisi na mashirika ya kigeni watatoa heshima zao za mwisho katika uwanja wa Nyayo.
Mazishi rasmi ya Rais mstaafu Mwai Kibaki yanatarajiwa kufanyika Jumamosi Aprili 30 mwaka huu huko Nyeri.
Mazishi hayo yataongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na yataendeshwa kwa heshima za kijeshi.