Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew kwa kushirikiana Wakazi wa jimbo la Bariadi Magharibi mkoani Simiyu, wamechimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa jimbo hilo.
Mhandisi Kundo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi amechangia mifuko 100 ya saruji na kuahidi kutoa mifuko mingine 50 na mabati ili kufanikisha ujenzi wa nyumba hiyo.
Mhandisi Kundo amesema ushiriki wake katika kazi hiyo ya ujenzi ni ishara ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo Wananchi wanashirikiana na Viongozi wao, badala ya kusubiri Serikali iwafanyie kila kitu.