Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuandaa filamu nyingine ya Tanzania The Royal Tour, akiomba itumike kutangaza maeneo ya uwekezaji pamoja na sekta ya kilimo na ufugaji wa nyuki mkoani humo.
Wakasuvi ametoa ombi hilo wakati wa uzinduzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa kilomita 342.9 inayounganisha mikoa ya Tabora na Katavi.
Wakasuvi pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza kima cha chini cha mishahara ya wafanyakazi kwa asilimka 23.3.
Barabara hiyo ya Tabora – Koga – Mpanda iliyojengwa kwa kiwango cha.lami, imezinduliwa na
Rais Samia Suluhu Hassan.
Ujenzi wa barabara hiyo umegharibu zaidi ya shilingi bilioni 470, fedha ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Ujenzi hio ulianza mwezi Machi mwaka 2018 na kukamilika mwezi Desemba mwaka 2019.