Wakandarasi watakiwa kukamilisha miradi kwa wakati

0
200

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amewataka wakandarasi wanaopewa tenda kutoka Wizara hiyo kukamilisha miradi kwa wakati na yenye ubora ili kutokwamisha maendeleo ya Tanzania ya Kidijitali.

Mhandisi Kundo ametoa kauli hiyo akiwa kitika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutoka Manyoni mpaka Itigi mkoani Singida alipokuwa akiongea na wasimamizi wa mradi huo wa ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unaosimamiwa na Kampuni ya kizalendo ya Raddy Fiber baada ya kampuni hiyo kuchelewa kumaliza mradi huo kwa wakati uliopangwa.

Amesema kuwa kitendo cha kampuni nyingi zinazochukua tenda za ujenzi wa miundombinu ya Mawasiliano kutoka Wizara hiyo kuchelewesha kukamilisha kazi hizo wakisingizia Uviko-19 sío sawa kwani ugonjwa huo sio sababu ya kuchelewesha mradi wakati shughuli nyingine zimekuwa zikifanyika japokuwa kulikuwa na wimbi la mripuko wa ugonjwa huo capo awali na kuwataka wasimamizi hao kuonyesha uzalendo katika miradi hiyo kwani Serikali iliwaamini kwa kutumia watu kutoka ndani ya nchi.

“Naomba Wakandarasi wote nchi nzima ambao wamebahatika kupata mikataba na kupata kazi ndani ya Wizara yetu naomba wakazingatie muda, wakazingatie kiwango na ubora ambao sisi tunauhitaji kutoka kwao na hii maana yake ni nini wakienda kufanya kazi na kuwasilisha mradi ulio kaika obora na viwango na mda uliotengwa maanayake wanaenda kujenga CV na makampuni mengine mengi ya ndani yataaminiwa na Serikali na Uchumi wa Nchi yetu hii utaimarika sababbu fedha hizi zitaendelea kubaki hapa hapa.”-amesema Mhandisi Kundo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa amemshukuru Naibu Waziri kwa ziara hiyo na kuwapatia watu uelewa juu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi na kuahidi Wilaya yake itaisimamia vizuri muundombinu huo.