Waislamu wahimizwa kushiriki Sensa

0
143

Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir amewahimiza Waumini wa dini ya Kiislamu kote nchini kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Msikiti wa Jumi’ Ul Istiqaama uliopo mkoani Kagera, Mufti ametoa agizo kwa masheikh na Maimamu kuanzia ngazi ya kata kuhamasisha Waumini wao kushiriki katika Sensa.

“Ndugu zangu Waislamu napenda kuwaasa kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi mwezi Agosti mwaka huu, kuhesabiwa kumeandikwa katika vitabu vyote vya dini hivyo kila mmoja ajitokeze kuhesabiwa” amesema Mufti

Aidha, amemumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuisaidia Jumuiya ya Istiqaama katika jitihada zake za kuendeleza misikiti na kuwaletea wananchi maendeleo.