Wahimizwa kuweka nguzo za majina kwenye mitaa

0
228

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amezitaka taasisi zinazoshughulikia miundombinu nchini kutekeleza ipasavyo maelekezo ya Serikali ya kuweka nguzo zenye majina ya barabara wanayoihudumia.

Mhandisi Kundo ameyasema hayo mkoani Mara, wakati akiendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa zoezi la anwani za makazi linalofanyika nchi nzima.

“Nisisitize uongozi wa mkoa wa Mara kusimamia utekelezaji wa maelekezo kuhusu operesheni ya anwani za makazi na kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji wake amoja na kushiriki utekelezaji, niwahimize viongozi, taasisi na wananchi wote kutumia mfumo huu utakapokamilika ili kwa pamoja tuone faida ya mfumo huu.” amesema Mhandii Kundo.

Aidha Mhandisi Kundo amewaomba Wananchi wa mkoa wa Mara kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa zoezi hilo kwani lina manufaa na linagusa maisha ya kila mmoja.

Zoezi la anwani za makazi linafanyika nchi nzima ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha mitaa yote inafahamika kiteknolojia, ili kuendana na kasi ya maendeleo