Wahandisi 12 wa TANROADS Morogoro wasimamishwa kazi

0
380

Rais John Magufuli amewasimamisha kazi kuanzia leo, wahandisi 12 wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Morogoro wanaohusika na ukaguzi wa barabara kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo mara baada ya kutembelea eneo hilo akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma.

Aidha, amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo lililokatika na kusababisha kukosekana kwa mawasilino kati ya mikoa ya Morogoro na Dodoma unakamilika ndani ya kipindi cha siku saba kuanzia leo.