Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mwanza imewakamata wahamiaji haramu 101 kutoka mataifa 10 duniani.
Kamishna Msaidizi Afisa Uhamiaji mkoa wa Mwanza, Peter Mbaku amesema wahamiaji hao wamekamatwa kufuata oparesheni maalum ya kuwabaini kuwakama na kuwachukulia hatua wahamiaji haramu hapa nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari Mbaku amesema ni raia wa nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Sudan Kusini, Pakistan na Misri.
Amesema wameshaanza kuwachukulia hatua wahamiaji hao haramu kwa kuwafikisha mahakamani, na baada ya hapo watarudishwa nchini mwao.