Idara ya Uhamiaji mkoani Mwanza imewakamata zaidi ya Wahamiaji Mia Moja, kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa idara hiyo, Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Mwanza, -Selemani Kameya amesema kuwa wahamaji hao wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ya jumla ya Shilingi Milioni 92.
kameya amesema kuwa katika kukabiliana na wahamiaji mkoani humo, Idara ya Uhamiaji imepekeka maafisa wa Idara hiyo katika kata zote za jiji la Mwanza na kuanzisha Rejista katika kata zinazoonekana kuwa na wahamiaji wengi.
Kwa mujibu wa Kameya, Idara ya Uhamiaji ya mkoa huo imeligawa Jiji la Mwanza katika Kanda Nne ili kuimarisha udhibiti wa Wahamiaji.