Wagonjwa wa Corona wafikia 88

0
333

Idadi ya wagonjwa waliothibitika kuwa na maambukizi ya covid-19 imefikia watu 88, ongezeko hili la wagonjwa linajumuisha wagonjwa wapya 6 waliotolewa taarifa na waziri wa afya wa zanzibar na wagonjwa wengine 29 kutoka bara.

Aidha wagonjwa waliopona hadi leo ni 11 huku vifo vilivyotokana na virus vya covid-19 vimefikia 4.

Serikali inaendelea kuwataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kama vyombo vya habari vinavyotoa taarifa na elimu kuhusu ugonjwa huo