Chama cha ushirika cha ukusanyaji wa maziwa wilaya ya Rungwe (MUAMARU), kimekabidhi vifaa vya kuhifadhia maziwa zaidi ya mia mbili vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na sita kwa wanachama wa chama hicho.
Vifaa hivyo vimetolewa na MUAMARU kwa lengo la kunusuru uharibifu wa maziwa yaliyokuwa yakikusanywa na wafugaji hapo awali.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho unaohusisha wanachama zaidi ya mia tatu, Afisa ushirika mkoa wa Mbeya Angela Maganga amesema Serikali imetoa asilimia kadhaa katika kuhakikisha kila mkulima anapatiwa chombo hicho.