Wafanyakazi wa TBC kuwania tuzo za EJAT

0
234

Watendaji wanne wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wameteuliwa kushindania tuzo za Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania/ Excellence in Journalism Awards Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2019.

Walioteuliwa kwa upande wa TBC1 ni Agness Mbapu na Tatu Abdallah Kazimoto. Kwa upande wa redio ni Joseline Joseph Kitakwa (TBC FM) na Betty Tesha (TBC Taifa).

Tuzo za EJAT hutolewa kwa waandishi wa magazeti, televisheni, redio na wa mitandaoni kwa kuwasilisha kazi zao bora zisizozidi tatu zinazopitiwa na EJAT kabla ya majina kutangazwa.