Wadau waendelea kutoa msaada Hanang

0
283

Wakati Serikali ikiendelea kutoa huduma mbalimbali za kiutu kwa waathirika wa Maporomoko ya Udongo yaliyotokea wilayani Hanang mkoani Manyara, wadau mbalimbali nao wanajitokeza zaidi kutoa faraja na kurejesha tabasamu kwa familia, ndugu na jamaa waliofikwa na madhila ya tukio hilo.

Meneja Masoko na Uhusiano wa Umma wa Amsons Group, Bhoke Rioba, amewasilisha msaada wa kampuni hizo wa hundi ya Shilingi Milioni Mia Moja (Tsh. 100m) kutoka Camel Cement, Magodoro 100, Mashuka 100 na Maduvet 100 kwa viongozi wa serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel na Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.