Wadau na waombolezaji mbalimbali wakisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi za Azam Media kwenye shughuli ya kuwaaga wapendwa watano wa Azam Media Limited waliotangulia mbele za haki jana Jumatatu, Julai 8, 2019.
Waliofariki kwenye ajali ya gari iliyotokea kati ya Shelui na Igunga. Ajali hiyo iletokea wakiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya kwenda kuonesha shughuli ya uzinduzi wa mbuga iliyopo Chato chini ya usimamizi wa TANAPA ambapo mgeni rasmi ni Rais John Magufuli