Wananchi wa kijiji cha Rungemba kilichopo katika halmashauri ya mji wa Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa, wamejenga wodi ya mama na mtoto itakayokuwa na chumba cha upasuaji katika zahanati ya kijiji hicho.
Wananchi hao wamejenga wodi hiyo kwa kuchangia nguvu zao baada ya kuchoshwa na usumbufu waliokuwa wakiupata wa kutembea umbali mrefu na kutumia gharama kubwa kwenda kufuata huduma za matibabu.
Kwa kutambua mchango wa Wananchi wa kijiji hicho cha Ringemba, Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi, ameendelea kukusanya nguvu kwa Wadau wa maendeleo, kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa wodi hiyo ili iweze kutumika.
Chumi amekabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa kijiji hich, lengo likiwa ni kusaidia kukamilisha ujenzi wa wodi hiyo.ulioibuliwa na Wananchi.