Waandishi wa habari wahimizwa kuchanjwa

0
198

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa, Jonathan Budenu kuhakikisha waandishi wa habari wote mkoani humo wanachomwa chanjo ya UVICO-19.

Malima ametoa agizo hilo wakati akizindua zoezi la chanjo mkoani Tanga lililofanyika kimkoa katika Hospitali ya Bombo.

“Ijapokua jambo hilo ni hiari lakini kutokana na asili ya kazi ya wanahabari jambo hilo linaonaekana kama ni lazima kwa ajili ya usalama wao,” ameeleza Malima.

Kwa mkoa mzima wa Tanga jumla ya chanjo 7,000 zimetolewa ili kusambazwa kwenye halmashauri zote 11 za mkoa huo.

Na Bertha Mwambela, Tanga