Wanandoa kizimbani kwa kudaiwa kutoa maneno chonganishi kuhusu corona

0
401
[09:14, 4/22/2020] Dix: Boniphace Mwita na mke wake Rosemary Jenera walipokiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa kesi yao.

Wanandoa wakazi wa Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kutoa lugha hatarishi kwa lengo kupotosha jamii kuhusu ugonjwa wa Corona.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wankyo Simon amesema kuwa kuwa Machi 20 mwaka huu Boniphace Mwita (49) na mke wake Rosemary Jenera (41) washtakiwa hao wakiwa kwenye daladala pamoja na abiria wengine, walitoa matamshi hatarishi kwa nia ya kupotosha umma wa Watanzania yanayosema “Ugonjwa wa Corona serikali inadanganya hakuna ugonjwa wowote na imefunga mashule kwa kuwa haina hela na ada za kusomesha watoto bure.”

Jamhuri imeiambia mahakama kuwa matamshi hayo yangeweza kuleta hofu au hisia mbaya dhidi ya nchi yao ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wameachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na itakuja tena Mei 6 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.