Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imejitoa kwenye udhamini wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kufuatia hasara iliyoipata.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Hisham Hendi, amesema wamefikia uamuzi huo kufuatia hasara waliyoipata, ambapo kwa mujibu ripoti ya fedha ya mwaka 2020/2021 kampuni hiyo imepata hasara ya shilingi bilioni 30.
Amesema kutokana na hasara hiyo, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imelazimika kusitisha udhamini huo.