VITUO VYA POLISI KUJENGWA KWA MICHANGO YA WANANCHI

0
144

Rais Samia suluhu Hassan amesema anatambua mafanikio yanayopatikana kupitia Jeshi la Polisi kwa Wananchi hasa utaratibu wa Polisi Kata, hivyo amemuelekeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni kukutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuwa na mkakati wa kuzishirikiaha halmashauri kujua wajibu wao katika kufanikisha ujenzi wa vituo vya Polisi vya kata.

Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika mkoani Dar es Salaam.

Amesema ikiwa Wananchi watashirikishwa katika upatikanaji wa vituo vya Polisi vya kata, itarahisishwa zaidi upatikanaji wake kuliko kuiachia wizara kubeba jukumu hilo peke yake.

Rais Samia ameongeza kuwa ikiwa Wananchi watashirikishwa na kuona ipo haja wanaweza kufanya peke yao, akitoa mfano wa Kizimkazi, Zanzibar ambapo kulikuwa na uhitaji wa muda mrefu wa kituo cha Polisi ila baada ya Wananchi kushirikishwa kituo hicho kimejengwa na hivi karibuni gari limekabidhiwa kwa kituo hicho ili kusaidia majukumu yake.