Viongozi watakiwa kuyaelewa mabadiliko

0
153

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa mikoa, wilaya na Makatibu Tawala kuyaelewa na kuendana na mabadiliko yanayotokea duniani na nchini, ili kuleta maendeleo yenye tija.

Amesema vipo visababishi vilivyopelekea mifumo ya ulimwengu kubadilika kiuchumi na kisiasa na kutaja magonjwa na vita, na kusema mabadiliko hayo yameleta mifumo mipya duniani ambayo inazitaka nchi za Afrika kujitegemea.

Akifunga mafunzo wa Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha mkoani Pwani Rais Samia amesema, ni vema kuendana na mabadiliko hayo bila ya kusubiri kulazimishwa kubadilika.

Rais Samia amewasisitiza viongozi hao kuwa na ndoto huku akifafanua kuwa ni heri kuwa mfungwa wa ndoto kwani ipo siku zitatimia kuliko kukaa bila ya ndoto.