Viongozi walioteuliwa karibuni waapishwa

0
1334

Rais John Magufuli amewaapisha Majaji Sita wa Mahakama ya Rufani na Majaji Kumi na Watano wa Mahakama Kuu aliowateua hivi karibuni.

Majaji wa Mahakama ya Rufani walioapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam ni Sahel Barke, Jaji Mary Levira, Jaji Rehema Sameji,  Jaji Winnie Korosso, Jaji Ignus Kitusi na Jaji Lugano Mwandambo.

Majaji walioapishwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ni pamoja na Cyprian Mkeha, Jaji Dunstan Ndunguru, Jaji Mwinshehe Kulita, Jaji  Ntemi Kilikamajenga,  Jaji Zepherine Galeba na Jaji Juliana Masabo.

Majaji wengine walioapishwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ni Mustapha Ismail,  Jaji Upendo Madeha,  Jaji Willbard Mashauri,  Jaji Yohane Masara,  Jaji Lilian Mongella,  Jaji Fahamu Mtulya,  Jaji John Kahyoza, Jaji Athumani  Kirati na Jaji Susan Mkapa.

Katika hafla hiyo,  wakuu wa wilaya mawili na Wakurugenzi Kumi wa halmashauri za wilaya ambao pia waliteuliwa na Rais Magufuli Januari 27 mwaka huu, nao wamepatiwa maelekezo ya kikazi na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma.

Wakurugenzi hao wa halmashauri za wilaya walioteuliwa ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi ni pamoja na Isaya Mbenje anayekwenda halmashauri ya  Pangani, Dkt Fatuma Mganga halmashauri ya  Bahi, Regina Bieda, -Tunduma, Jonas Mallosa halmashauri ya Ulanga, Ally Juma Ally anayekwenda Njombe  na  Misana Kwangura halmashauri ya Nkasi.

Wengine ni Diodes Rutema halmashauri ya Kibondo, Netho Ndilito halmashauri ya Mufindi, Elizabeth Gumbo halmashauri ya Itilima na Stephen Ndaki anayekwenda halmashauri ya Kishapu.

Wakuu wapya wa wilaya ambao nao wamepatiwa maelekezo ya kikazi na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma Ikulu jijini Dar es salaam ni Charles Kabeho aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara na Thomas Apson ambaye anakua mkuu wa wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.