Viongozi Wakuu wa Wizara ya Habari watekeleza agizo la Rais.

0
198

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi wamekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba kuhusu namna ambavyo Michezo ya Bahati Nasibu (Sport Betting Nationary Lottary) inavyoweza kuchangia maendeleo ya michezo na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Hatua hii ni mkakati mahusus wa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan la kutaka kuzalisha ajira kwa vijana kupitia Michezo na Sanaa kwa kuwa ni miongoni mwa sekta zinazotoa ajira kwa vijana wengi Tanzania.

Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 27, 2021 katika Ukumbi wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma.