Viongozi wa Umma wanaotumia madaraka vibaya kushughulikiwa

0
295


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dakta Mary mwanjelwa  amewaagiza makamishna wa tume ya utumishi wa umma kuanza kuwashughulikia viongozi wanaotumia madaraka vibaya kwa lengo la kurudisha nyuma  sekta ya utumishi wa umma.

Akifungua  mafunzo elekezi kwa makamishna hao wateule Dakta  Mwanjelwa amesema wakati serikali ikiendelea na mkakati  wake wa kuleta mapinduzi ya  uchumi wa viwanda lazima watumishi wa  umma wafahamu kuwa wanahitajika kuwa wabaunifu kiutendaji ili kufikia malengo hayo kwa kuchapa.

Dakta Mwanjelwa pia amewataka makamishna hao kutumia nafasi yao kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya umma  ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za waajiri na wafanyakazi  kwa wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume a Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Dakta Stephen bwana amesema kuwa atahakikisha  matatizo yanayoikabili sekta ya umma yanapatiwa  ufumbuzi wa haraka .

Tume ya Utumishi wa Umma iliyoteuliwa hivi karibuni na Rais John  Magufuli itakuwa na majukumu ya kushughulikia kero zinazoikabili sekta ya umma .