Viongozi wa Dini wakumbushwa kuendelea kulinda maadili

0
71

Viongozi wa dini, mila na watanzania wote wamekumbushwa kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili, ili kuwa na Taifa lenye maadili mema.

Hayo yamesemwa mkoani Dar es Salaam na Azim Dewji ambaye ni Mwenyekiti wa wadhamini wa viongozi wa dini wa kamati za amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania, wakati wa ufunguzi wa kongamano la kitaifa la maadili la viongozi wa dini wa kamati za Amani na Jumuiya ya maridhiano Tanzania.

Dewji amesema Tanzania kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wake Dkt. Philip Mpango na wasaidizi wao ni mpango wa Mungu, hivyo kila mtanzania anapaswa kuwapa ushirikiano katika kutimiza majukumu yao ya kulijenga Taifa.

Kongamano hilo la kitaifa la maadili la viongozi wa dini wa kamati za Amani na Jumuiya ya maridhiano Tanzania limefunguliwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.