Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za kuratibu maandamano.
Akizungumza na TBC, Kamanda Lazaro Mambosasa ameeleza kuwa licha ya viongozi hao kusema kuwa maandamano hayo ni ya amani, lakini wamebaini uwepo wa vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibufu wa mali za wananchi.
Amewataja viongozi wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni Freeman Mbowe, Godbless Lema na Boniface Jacob.