Viongozi wa CCM ziarani China

0
143

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo anaendelea na ziara ya kikazi nchini China, akiwa amefuatana na viongozi wengine wa chama hicho.

Viongozi hao ni pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya NEC, wenyeviti wa mikoa wa CCM na wenyeviti wa Jumuiya zilizo chini ya Chama Cha Mapinduzi.

Ziara hiyo iliyoanza Aprili 16, 2023 itamalizika Aptili 26, 2023, huku ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Kikomonisti Cha China (CPC).

Uhusiano kati ya CCM na CPC uliasisiwa na waanzilishi wa vyama hivyo na kuendelea kuimarishwa na viongozi wa sasa.