Vijiji vya Kwanyange na Kivisini vyapata maji safi

0
192

Wakazi vijiji vya Kwanyange na Kivisini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wameishukuru Serikali kwa kuwajengea mradi wa maji safi na salama.

Wakizungumza na TBC wakati Mwenge wa Uhuru ukizindua mradi huo wakazi hao wamesema walikuwa wakilazimika kunywa maji ya kwenye makorongo kutokana na kukosa maeneo ya kuchota maji.Wamesema wakati mwingine walilazimika kwenda eneo la Kifaru kufuata huduma ya maji safi na salama.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji unaohudumia wakazi takribani 1,500 wa vijiji hivyo vya Kwanyange na Kivisini wilayani Mwanga, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava ameagiza kuimarishwa kwa ulinzi katika tenki la maji la mradi huo.