Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amewataka vijana kuwa mabalozi wa kutangaza kazi nzuri inayofanywa na Serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan.
Waziri Bashungwa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Karagwe mkoani Kagera ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vijana kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Karagwe, katika kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM la wilaya hiyo.
“Vijana hakikisheni mlipo mama Samia awepo, tuna sababu ya kutembea kifua mbele kama vijana tukiinadi kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mama Samia kwa sababu wote tunaona kwa macho namna kazi inavyoendelea kisawasawa.” amesema Waziri Bashungwa
Kikao hicho cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM wilayani Karagwe ni cha kikanuni kwa ajili ya kufanya tathmini ya kazi za Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ndani ya wilaya hiyo.